Umoja wa Afrika(AU) yenye makao yake makuu Addis Ababa, nchini Ethiopia imepanga kuchangisha fedha ili kuziwezesha nchi za pembe ya afrika.
AU ambayo imepanga kukutana hivi leo itawakutanisha viongozi wa Afrika kutoka nchi wanachama huku lengo likiwa ni kukusanya dola bilioni moja na nusu kukabiliana na janga la njaa kwenye nchi hizo ambazo ni Somalia, Djibout, Eritrea, Ethiopia na Sudan.
Mkutano ambao ni wa kwanza wa aina hiyo utaongozwa na mwenyekiti wake, Bw. Jean Ping.
Mbali na nchi zaMarekani, Brazili,China, Uingereza,Japan, Uturuki na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu(OIC) kutoa misaada, lakini, umoja huo umelalamikiwa kwa kuchelewesha misaada kwa wakazi wa maeneo hayo.
Janga hili linasemwa kuwa kubwa tangu kutokea kwa hali kama hiyo mwaka 1991-1992 huko nchini Somalia.
No comments:
Post a Comment