Ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba mizigo kuelekea ukanda wa kimataifa wa bahari imepata ajali eneo la pwani ya Siberia, maafisa wa masuala ya dharura nchini wamesema hivi leo. Ndege hiyo ya mizigo ilitua nchini Kazakhstan saa moja kutokea Baikonur Cosmodrome, ikiwa karibu na kutua.
Timu ya waokoaji imepelekwa eneo la tukio, tawi la Masuala ya Dharura la ukanda huo lilisema, huku maafisa hao wakisita kusema kama ajali hiyo imesababisha madhara yeyote hadi sasa wakati taarifa za uchunguzi zikisema ndege hiyo imepata ajali eneo la ukanda wa Altai.
Mapema jumatano hii shirika la masuala ya anga cha nchini Urusi la Roscosmos limeripoti kwamba ndege hiyo ya mizigo ilipoteza uelekeo mara baada ya kuondoka hivyo kupotea njia yake na kuipotea rada.
Popular Posts
8.24.2011
WAASI WAZIDI KUMWANDAMA KANALI GADAFFI
Waasi wa nchini Libya wameendeleza mashambulizi dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muhamar Gadaffi huku safari hii wakiahidi kutoa kitita kinono kwa yeyote atayefanikisha kukamatwa kwa kiongozi huo.
Wakati huo nchi za magharibi zinatazamiwa kutoa mabilioni ya fedha kwa waasi hao ili kufanikisha oparesheni dhidi ya wanayemwita dikteta yaani "kanali Gadaffi" , wakati hayo yakijiri yeye mwenyewe kanali gadaffi amedai waasi hao wangefikia suluhisho mapema endapo mabepari wa magharibi wangeuchia Umoja wa Afrika kutafuta muafaka wa tatizo hilo.

Subscribe to:
Comments (Atom)