Waasi wa nchini Libya wameendeleza mashambulizi dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muhamar Gadaffi huku safari hii wakiahidi kutoa kitita kinono kwa yeyote atayefanikisha kukamatwa kwa kiongozi huo.
Wakati huo nchi za magharibi zinatazamiwa kutoa mabilioni ya fedha kwa waasi hao ili kufanikisha oparesheni dhidi ya wanayemwita dikteta yaani "kanali Gadaffi" , wakati hayo yakijiri yeye mwenyewe kanali gadaffi amedai waasi hao wangefikia suluhisho mapema endapo mabepari wa magharibi wangeuchia Umoja wa Afrika kutafuta muafaka wa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment